14 Yesu kwa imani


1. Yesu kwa imani,
Nakutumaini,
Peke yako;
Nisikie sasa,
Na kunitakasa,
Ni wako kabisa
Tangu leo.
 
2. Nipe nguvu pia
Za kusaidia
Moyo wangu;
Ulikufa wewe,
Wokovu nipewe
Nakupenda wewe,
Bwana wangu.
 
3. Hapa nazunguka
Katika mashaka,
Na matata;
Palipo na giza
Utaniongoza
Hivi nitaweza
Kufuata.
 
4. Takuwa mzima
Nivushe salama
Mautini;
Sina hofu kamwe
Ukiwapo nami
Nami nikwandame
Siku zote. 

Comments