83 Kwa wingi wa nyama
1. Kwa wingi wa nyama,
Na sadaka pia,
Hupata wapi salama,
Kwondoa hatia?
2. Sadaka ni Yesu,
Hwondoa makosa;
Dhabihu mwenye jina kuu,
Atanitakasa.
3. Kwa yangu imani,
Nikuweke sasa
Mkono mwako kichwani
Kukiri makosa.
4. Roho yakumbuka
Mambo ya mtini,
Mzigo ulijitweka,
Ndiyo yangu deni.
5. Deni hutanguka,
Tukimuamini;
Kwa damu tumeokoka,
Twimbe furahani.
Comments
Post a Comment