66 Po pote mashamba yajaa


1. Po pote mashamba yajaa,
Tele nafaka pevu,
Po pote yang’aa meupe
Bondeni na nyandani.

Mwenye mavuno, wasihi
Upeleke wavuni,
Wakusanye mazao,
Hata kazi iishe. 
 
2. Wapeleke uchaoni,
Waende na jotoni,
Mpaka jua lishukapo
Wakusanye ko kote.
 
3. Watenda kazi wa Bwana,
Mlete sasa mazao,
Na jioni ingieni
Kwake na furaha kuu. 

Comments

Popular posts from this blog

23 Ni salama rohoni mwangu

7 Ni tabibu wa karibu

16 Kumtegemea Mwokozi