60 Waponyeni watu


1. Waponyeni watu wamo kifoni,
Watoeni walio shimoni;
Na aangukaye mumzuie;
Ya Bwana Yesu wahubirini. 
 
Walio kifoni waokoeni,
Mwokozi yuko, wahubirini. 
 
2. Wajapokawia anangojea,
Awasubiri waje tobani;
Msiwadharau, muwaonyeni;
Huwasamehe; wakiamini.
 
3. Myoyoni mwa ndani, yule shetani
Ameyaseta mawazo yao;
Lakini kwa Bwana huwa mazima,
Tukiwavuta kwa pole hao.
 
4. Kawaokoeni, wale njiani,
Mutimize mapenzi ya Bwana;
Na kwa nguvu zake warudi kwake,
Kwa subira waonyeni sana. 

Comments