94 Siku ya mbingu kujawa na sifa


1. Siku ya Mbinguni kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni. 
 
Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu. 
 
2. Na siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza msalabani;
Aliumia, aliaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.
 
3. Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni mwokozi, kwake twaokoka.
 
4. Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka kwa kushinda kwake,
Naye yuko milele Mbinguni.
 
5. Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi: wangu, tutaonana. 

Comments

Popular posts from this blog

23 Ni salama rohoni mwangu

7 Ni tabibu wa karibu

16 Kumtegemea Mwokozi