92 Nataka nimjue Yesu

 
1. Nataka nimjue Yesu,
Na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake, na
Wokovu wake kamili. 
 
Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue pendo lake, na
wokovu wake kamili. 
 
2. Nataka nione Yesu,
Na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni,
Kujidhihirisha kwangu.
 
3. Nataka nifahamu, na
Nizidi kupambanua
Mapenzi yake, nifanye
Yale yanayompendeza.
 
4. Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo zaidi,
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake. 
 
Shared from Tenzi za Rohoni app.
Click this link to download https://goo.gl/9HNM1M

Comments