146 Neno la Mungu takata
1. Neno la Mungu takata
Lililotoka mbinguni;
Ambalo moto na panga
Haziwezi kulishinda.
/:Twakushika siku zote
Maishani na kufani. :/
2. Waliotutangulia
Waliokutegemea,
Wamekufia mashujaa;
Nasi tulio watoto.
Twakushika …
3. Neno la Mungu takata,
Tukushuhudie nasi
Kwa neno tamu na tendo
Kunako wenzi au adui.
Twakushika …
Comments
Post a Comment