134 Juu yake langu shaka


1. Juu yake langu shaka,
Yesu namuwekea,
Nami sitafedheheka
Nikimtegemea. 
 
Natumai, natumai,
Nnatumai kwake tu;
Natumai, natumai,
Natumai kwake tu. 
 
2. Juu yake, dhambi zangu;
Aniosha kwa damu;
Nionekane kwa Mungu,
Nisiye na laumu.
 
3. Juu yake yangu hofu;
Kwake nimetulia;
Sipotei kwa upofu
Njia aning’azia.
 
4. Juu yake raha yangu;
Humuangalia tu;
Mwenye kila ulimwengu,
Aniruzuku na huu.
 
5. Juu yake, moyo wangu;
Hali yangu na mali;
Mimi wake, Yeye wangu,
Twapasana kamili.

Comments

Popular posts from this blog

23 Ni salama rohoni mwangu

7 Ni tabibu wa karibu

16 Kumtegemea Mwokozi