100 Tumrudie Bwana


1. Mbona washangaa njiani?
Mbona warejea nyuma?
Warudi tena gizani
Alimokutoa Bwana? 
 
2. Ni ya bure yote haya,
Uliyofunzwa ya Mungu?
Ni bure amekufia
Bwana Yesu kwa uchungu?
 
3. Wamtia kristo aibu
Na maneno yake pia?
Siku yaja ya hesabu,
Utamjibuje Bwana?
 
4. Upandapo tena hayo,
Halafu utayavuna.
Rudi kwa Bwana upesi,
Mwombe akupokee tena. 

Comments

Popular posts from this blog

23 Ni salama rohoni mwangu

7 Ni tabibu wa karibu

16 Kumtegemea Mwokozi